Wananchi Kipunguni kulipwa fidia mwezi ujao

Na Nora Damian

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema fidia kwa wakazi wa Mtaa wa Kipunguni wanaotakiwa kuhama kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, zitaanza kulipwa Agosti mwaka huu.

Akizungumza leo Julai 8,2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Segerea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Liwiti, amesema imechelewa kwa sababu ya dharura iliyojitokeza katika mwaka wa fedha uliopita (2023/2024).

Dk. Nchemba alikuwa akizungumza kwa simu baada ya kupigiwa na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Amos Makala, kutoa majibu ya suala hilo lililoulizwa na wananchi katika mkutano huo.

“Jambo la Kipunguni ninalifahamu vizuri na nilishafika Kipunguni kulielezea, tulitoa kauli ya serikali. Mheshimiwa mbunge (Bonnah) amelifuatilia mara nyingi, amelifikisha kwenye vikao kadhaa vya viongozi wakuu na vyote kauli ya serikali ilikuwa ni kuanza kulipa fidia mara moja.

“Tumechelewa tofauti na tulivyoahidi kwa sababu ya dharura iliyojitokeza katika mwaka wa fedha uliopita, tullikuwa na dharura kubwa ambazo zilikuwa zinalikata taifa vipande vipande yakiwemo mafuriko ya Kusini.

“Leo asubuhi nilikutana na ujumbe wa viongozi 10 kutoka Kipunguni, niliwapa majibu kwamba baada ya kuanza mwaka mpya wa fedha tunatarajia mwezi mmoja utatumika kuweka sawa mifumo mipya ya malipo…tunatarajia kuanzia mwezi wa nane tuanze kulipa wananchi wa Kipunguni,” amesema Dk. Nchemba.

Makala ambaye alikagua utekelezaji wa Ilani katika miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa shule za sekondari amempongeza Bonnah na kusema ni mchapakazi.

“Bonnah anafanya kazi, mambo ya kusema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni…ukishamnyonga haki anaipata wapi…kwahiyo tunakupongeza sana kwa kazi nzuri unayoifanya. Ni kamanda mzuri, yuko na wananchi wake na anawatetea muda wote.

“Kila waziri atakayeteuliwa awe wa ujenzi au uchukuzi anajua kuna swali la Kipunguni, lazima amuulize. Ameliweka vizuri suala hili na sasa yamebaki malipo, mimi shahidi wenu mwezi wa nane wananchi watapata fidia zao,” amesema Makala.

Awali Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, amesema kwa muda mrefu wananchi wa Kipunguni wamekuwa wakiahidiwa kulipwa fidia bila mafanikio na kuiomba serikali kuharakisha malipo hayo.

spot_img

Latest articles

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...

Hivi vikosi kazi vimerejea kwa mlango wa nyuma?

KUNA kila dalili kwamba taifa letu kidogokidogo linakumbwa na hali ya kutokuaminiana. Hali hii...

More like this

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...