Mzee miaka 63 kizimbani kwa kumbaka binti yake

Na Malima Rubasha, Serengeti

Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, imempandisha kizimbani Marwa Masegwe(63) mkazi wa Kijiji cha Kibeyo Kata ya Kisangura kwa kosa la kumbaka binti yake wa kuzaa mwenye umri wa miaka 10 usiku Mei 15 na 16,2024 maeneo ya nyumbani kwake.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Joseph Mohere, akisoma hati ya mashtaka ameiambia mahakama hiyo kuwa katika kesi jinai namba 14565 ya mwaka 2024, mshtakiwa Marwa Mwita Masegwe mwenye umri wa miaka 63 mkazi wa kijiji cha kibeyo wilayani Serengeti alimbaka binti wa miaka 10 ambaye ni mtoto wake wa kuzaa, siku ya Mei 15 na 16 mwaka huu majira ya usiku nyumbani kwake katika kijiji cha kibeyo.

Hakimu Mohere aliendelea kuieleza mahakama kuwa hali hiyo ilipelekea binti huyo(jina limehifadhiwa) kutoa taarifa kwa majirani ili apate msaada kuhusu kitendo alichofanyiwa na baba yake kwa kuwa walikuwa wanaishi yeye na mdogo wake wa kiume na baba yao mzazi bila kuwepo kwa mzazi mwingine.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Nico Malekela pamoja na Paul Mlelwa umedai kuwa upande wa Jamhuri una mashahidi wanne na kati yao mashahidi watatu ni kutoka Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Serengeti, Mganga kutoka hospitali ya Wilaya na Mhanga mwenyewe ambaye ni binti huyo na kwamba mashahidi wametoa ushahidi pasipo shaka yoyote.

Hata hivyo kwa upande wa mshtakiwa alipotakiwa kujitetea dhidi ya kesi hiyo inayomkabili alikana kuhusika kutenda kosa hilo.

Shauri hilo limeahairishwa hadi Juni 17, 2024 hadi kesi itakapotajwa tena na mshtakiwa amerudishwa rumande.

spot_img

Latest articles

JAB yawafungia watangazaji wanne wa kipindi cha Genge la GEN TOK kwa kukiuka maadili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewafungia...

Madai ya dada wa Polepole kubebwa, Polisi yachunguza 

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limesema limepokea taarifa za...

Kiungo Moussa  Conte rasmi atambulishwa Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania, Klabu ya Yanga...

Tanzania kuwa na mashirika ya umma yenye ushindani ifikapo 2050

Na Mwandishi Wetu IFIKAPO mwaka 2050, Tanzania inajiona kuwa na Mashirika ya umma ya...

More like this