FCS, Vodacom Foundation wasaini makubaliano kuelekea Wiki ya AZAKI

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), na  Vodacom Tanzania Foundatio wamesaini makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Shilingi milioni 150 ikiwa ni  udhamini  wa Wiki ya AZAKI 2024, itakayofanyika Jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 13, mwaka huu.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, iliyofanyika leo Mei 21,2024, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge, amesema kiasi hicho cha fedha kimeongeza chachu ya ushiriano wa pamoja wa kukuza maendeleo ya jamii kupitia Wiki ya AZAKi.

Aidha, katika kufanikisha Wiki ya AZAKi, FCS wamechangia shilingi milioni 250, ambapo michango mingine inatoka kwa wadau wa maendeleo zikiwemo asasi za kiraia.

Rutenge amesema kuwa ili kuweza kusonga mbele sauti mbalimbali za wadau na wabia zinahitaji katika kuchochea mchakato wa maendeleo.

“Ili tuweze kusonga mbele na kuiona Tanzania tunayoitaka, sauti za wadau na wabia mbalimbali zinahitajika kusikika na ziwe sehemu ya kutoa mchango katika mchakato mzima wa maendeleo ambayo yatasaidia kujenga maono ya kulipeleka Taifa letu mbele” amesema Rutenge.

Ameeleza kuwa Sekta Binafsi ni wabia na wadau wakubwa wa maendeleo, nakwamba ushirikiano huo ni muhimu katika kubadilishana uzoefu huku akibainisha kuwa FCS wamekuwa wabobezi na wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Ushirikiano huu utasaidia kubadilishana uzoefu, Vodacom Foundation watanufaika na uzoefu tulionao katika kusimamia miradi ya maendeleo, kuchochea usawa wa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wanawake, vijana, watoto na watu wenye ulemavu. FCS nao watanufaika katika kuunganisha watu kwa kutumia teknolojia kwa kuzingatia nchi ipo kwenye mapunduzi ya teknolojia,” ameeleza Rutenge. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Foundation Tanzania, Zuweina Farah, amesema ili kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ushirikiano wa pamoja unahitajika kati ya AZAKi, Sekta Binafsi na Serikali.

Pia ameongeza kuwa, lengo la Vodacom Foundation Tanzania ni kukuza ushirikiano katika kuleta maendeleo ya jamii, kuimarisha utawala bora na kuboresha mazingira ya Biashara nchini.

Wiki ya AZAKi mwaka huu imebebwa na kauli mbiu ya isemaho ‘Sauti, maono na thamani’ ambayo inaambatana na lengo Kuu la FCS la kuwezesha maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

spot_img

Latest articles

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

Senegal yavuliwa ubingwa wa AFCON 2025, wapewa Morocco

Na Mwandishi Wetu SENEGAL imevuliwa ubingwa  wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada...

Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi...

Vijana 3,967 waomba uwezeshaji kupitia Go Green na IMBEJU ya CRDB Bank Foundation

Na Mwandishi wetu JUMLA ya vijana 3,967 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamewasilisha maombi ya...

More like this

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

Senegal yavuliwa ubingwa wa AFCON 2025, wapewa Morocco

Na Mwandishi Wetu SENEGAL imevuliwa ubingwa  wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada...

Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi...