Biden: Tendo la ndoa siri ya furaha kwenye ndoa

Rais Joe Biden wa Marekani amewaasa wasaidizi wake kwamba siri ya ndoa ya muda mrefu na ya kudumu ni “tendo la ndoa.” Kitabu kipya kuhusu mke wa rais, Jill Biden ambacho kinaangazia ndoa yao iliyodumu kwa miaka 47 sasa, kinalitaja ‘Tendo la ndoa’ kuwa ndio kirutubisho muhimu zaidi katika ndoa.

Kitabu hicho “American Woman – The Transformation of the Modern First Lady, from Hillary Clinton to Jill Biden,” kimeandikwa na mwandishi wa New York Times katika Ikulu ya White House, Katie Rogers na kinatarajiwa kutoka wiki hii.

Sehemu inayohusu ngono inachukua vifungu vichache tu katika kitabu hicho chenye kurasa 276, lakini tayari maudhui hayo yameibua mjadala mkubwa mitandaoni na kugonga vichwa vya habari sehemu mbalimbali duniani.

Jill Tracy Jacobs Biden, mke wa pili na wa sasa wa Biden, alizaliwa Juni 3, 1951. Alikutana na Biden Machi 1975. Kitabu hiki pia kinaelezea uchungu wa Biden alioupata baada ya mke wake wa kwanza, Neilia, kufariki katika ajali ya gari mwaka wa 1972 pamoja na binti yao Naomi.

Je unakubaliana na kauli hii ya rais Biden?

spot_img

Latest articles

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

More like this