Watanzania washinda milioni 234 za AGT, Rais Samia awapongeza

Na Mwandishi wetu

Wanasarakasi wawili watanzania ambao ni ndugu, Fadhil Ramadhani na Ibrahim Job, wameshinda kitita cha fedha cha dola za Kimarekani 250,000 sawa na sh 634 milioni baada ya kuibuka washindi wa American Got Talent (AGT) Fantasy League.

Watanzania hao wanaounda kikundi cha sarakasi kinachoitwa Ramadhani  Brothers, waliibuka washindi usiku wa jana Februari 19,2024 kwa kuwashinda wapinzani wao wengine tisa waliofika nao fainali.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram baada ya kutangazwa washindi katika usiku huo, wamesema ni ushindi wa kushangaza kwao na kuwashukuru wote waliowapa sapoti.

Wamesema wanajivunia  kutangazwa wabingwa wa dunia wa mashindano, huku wakiwapokeza washindani wenzao  ambao wamewafanya wawe bora zaidi.

Katika hatua nyingine Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza washindi hao kutokana na kuitangaza vema Tanzania.

“Pongezi kwa vijana wetu Fadhil na Ibrahim (The Ramadhan Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League, safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine,” amesema Rais Samia.

spot_img

Latest articles

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

Yanga yatua Zanzibar kuitengenezea dozi AS FAR Rabat

Na Winfrida Mtoi Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR...

Rais Samia atangaza Baraza Jipya la Mawaziri, nane watemwa

Tatu Mohamed na Winfrida Mtoi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,...

More like this