Watalii waongezeka Kilwa

Na Mwandishi wetu, Kilwa

Idadi ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani imezidi kuongezeka katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kutokana na utalii wa kihistoria na kiutamaduni.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA ),taasisi yenye dhamana ya usimamizi wa hifadhi hiyo, Februari 15,2024 ilipokea kundi la tani la watalii 119 kutoka ikiwa ni mfululizo wa safari za watalii wa nje kutembelea hifadhi hiyo kwa shughuli za utalii.

Watalii waliowasili ni kutoka katika nchi za Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ubelgiji, Hispania na Canada wakisafirishwa na meli iitwayo Le Bougainville.

Kwa mujibu wa TAWA, hayo ni matokeo ya hatua za makusudi zilizofanywa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha sekta ya utalii nchini inakua kwa kasi baada ya kucheza filamu maarufu iitwayo Tanzania The Royal Tour.

Pia jitihada za dhati zilizofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mamlaka hiyo kwa kuboresha miundombinu wezeshi ya utalii katika hifadhi hiyo.

spot_img

Latest articles

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

More like this