Wageni 300 kuwasili nchini kushiriki mkutano wa CISM

Ramadhan Hassan, Dodoma

Zaidi ya wageni 300 kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuwasili nchini kushiriki mkutano Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) utakaoanza Mei 12-19,2024 jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unakuwa wa pili kufanyika Tanzania ambapo mara ya mwisho ilikuwa 1991 jijini Arusha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 20,2024 jijini hapa, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo Meja Jenerali Francis Mbindi, amesema lengo la baraza hilo ni kutumia shughuli za michezo na utimamu wa mwili kama njia ya kueneza amani duniani.

“Ikiwa ni kuhamasisha mshikamano, urafiki, heshima, usawa, uadilifu na ushupavu,”amesema.

Amesema baraza hilo ni shirikisho la kimataifa lililoundwa Februari 18, 1945 baada ya vita kuu ya pili ya dunia na hadi sasa lina nchi wanachama 140 kutoka mabara yote duniani na Tanzania ilijiunga mwaka 1973.

“Tanzania tumepata dhamana ya kuwa wenyeji wa kuandaa mkutano huu wa 79 ambao utafanyika Dar es Salaam kuanzia May 12 hadi Mei 19, 2024,”amesema

Amesema mgeni rasmi siku ya ufunguzi Mei 13, 202 anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema siku ya kufunga Mei 17, 2024 mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Sababu zilizopelekea kuteuliwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu ni uwepo wa amani, ulinzi na usalama,”amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha amesema kiswahili ikiwa ni lugha ya Taifa itakuwa miongoni mwa lugha tano zitakazotumika kwenye mkutano huo ambapo zingine ni Kiingereza, Kihispania, Kifaransa na Kiarabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Michezo JWTZ, Kanali Martin Msumari amesema watakuwa na michezo ya kipaumbele ambayo ni pamoja na riadha,ngumi na michezo mbalimbali.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this