Umeme wa ardhini kumaliza kero Temeke

Na Nora Damian

Tatizo la kukatika kwa umeme lililokuwa linaikabili Wilaya ya Temeke limepata ufumbuzi baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme chini ya ardhi.

Ujenzi wa huo wa msongo wa kilovoti 132 unagharimu Sh bilioni 16 na unatarajiwa kukamilika Machi 2024.

Akizungumza leo Februari 20,2024 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kukagua miradi ya maendeleo, Meneja wa Tanesco Temeke, Ezekiel Mashola, amesema njia hiyo yenye urefu wa kilomita 6.8 itazalisha megawati 100.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme chini ya ardhi katika Wilaya ya Temeke.

“Tunajenga njia hii ili kuhakikisha miundombinu ya umeme hailemewi kwa wingi wa umeme. Hadi Machi 30,2024 mgawo wa umeme Temeke utaisha,” amesema Mashola.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila, amesema ongezeko kubwa la uwekezaji hasa viwanda na makazi ya watu umesababisha njia za kusafirisha umeme kulemewa kwa kuwa miundombinu ya umeme ni ileile.

Amesema kupitia mradi huo wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme utamaliza mgawo wa umeme ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara katika wilaya hiyo hasa siku za Jumamosi na Jumapili.

“Umeme unapokatika kuna sababu zaidi ya moja na msichukulie jambo hili kisiasa, tusijadili mambo kwa mihemko. Kazi kubwa inafanyika na Rais Samia ametoa fedha ambazo zinatumika kujenga njia za kusafirisha umeme chini ya ardhi ikiwemo hii inayofanyika hapa…ujenzi utakapokamilika umeme hautasumbua tena,” amesema Chalamila.

spot_img

Latest articles

Mavazi ya kitamaduni kivutio kingine AFCON 2025

Na Winfrida Mtoi SHAMRASHAMRA kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2025), zimezidi kupamba moto, hasa baada...

Livembe: Mchakato wa Uchaguzi ulikuwa wa haki na halali

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amesema mchakato wa...

Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda...

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

More like this