TPLB yavuna mamilioni Yanga, Simba

Na Winfrida Mtoi

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imevuna mamilioni kutoka katika klabu za Yanga, Simba na nyingine za ligi hiyo kutokana na makosa mbalimbali waliyofanya kwenye michezo yao iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya kikao cha kamati hiyo cha Februari 14,2024 cha kupitia mwenendo na matukio ya michezo ya Ligi, klabu ya Yanga imetozwa faini ya sh 1,000,000 kwa kosa la mashabiki wake watatu kuonekana kwenye vyumba vya kuvalia wakati wa mechi yao na Tanzania Prisons.

Klabu hiyo imetozwa faini nyingine ya sh 1,000,000 pamoja na Dodoma Jiji kutokana wachezaji wao kuchelewa kurejea uwanjani kipindi cha pili wakati timu hizo zilipokutana na kusababisha mchezo kuchelewa kwa dakika saba.

Mshambuliaji wa timu hiyo Clement Mzize ametozwa faini ya sh 1,000,000 kwa kosa la kuondoa taulo la kipa wa Dodoma Jiji lililokuwa golini hali iliyoashiria imani za kishirikina, huku Shomari Kibwana naye alipigwa faini kama hiyo kwa kosa linalofanana na hilo wakati wa mechi dhidi ya Mashujaa FC.

Kwa upande wa Simba imepigwa faini ya 1,000,000 kwa kosa la mashabiki wake kuonekana katika video za mitandaoni wakimwaga vitu nyenye asili ya unga kitendo kilichoashiria ushirikina siku moja kabla ya mchezo wao na Tabora United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Klabu hiyo imepigwa faini nyingine kama hiyo kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa za maji wakati wa mechi yao na Azam FC.

Klabu nyingine zilizotozwa na faini kama hiyo ni Mashujaa FC, Tanzania Prisons.

spot_img

Latest articles

Simba yaachia pointi tatu kwa Mkapa, Azam nayo mambo magumu

Na Winfrida Mtoi Simba imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kufungwa na Petro de Luanda bao...

Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuendeleza mchezo wa kuogelea

Na Winfrida Mtoi WADAU wa mchezo wakuogelea Afrika Mashariki wamekutana kujadili maendeleo ya mchezo huo,...

Ndejembi: Tanesco mmefanya mageuzi makubwa katika huduma ya umeme kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme Tanzania...

Dube awapa raha wananchi

Na Winfrida Mtoi BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama...

More like this