Papa Francis akutana na Rais Samia

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan huku wakieleza dhamira yao ya pamoja ya kuhimiza amani duniani.

Baba Mtakatifu Francisko amempokea Rais Samia na ujumbe, mjini Vatican siku ya Jumatatu. Baada ya kukutana na Baba Mtakatifu Francisko, Rais amekutana na Katibu wa Jimbo la Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Katibu wa Vatican anayeshughulikia Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu, Paul Richard Gallagher.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi Rasmi ya Mawasiliano ya Vatican (Holy See Press Office), viongozi hao wawili walikuwa na mjadala mzuri ambao pamoja na mambo mengine umeangazia uhusiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Vatican.

Kadhalika wamezungumzia “mchango muhimu ambao Kanisa Katoliki limekuwa likitoa nchini Tanzania hasa katika sekta za elimu na afya. Kadhalika wamezungumzia hali ya kikanda na mambo ya sasa ya kimataifa, na pande zote mbili zilielezea matakwa yao ya pamoja ya kuhimiza amani.

Chanzo: Vatican Radio

spot_img

Latest articles

YAPO MATAMANIO YA UCHAGUZI WA 2019 KUJIRUDIA 2024?

KUNA uhusiano wowote kati ya mafanikio ya kiuchumi kwa nchi yoyote na kukua kwa...

Dabi ya Kariakoo Wanawake, kitaumana kesho

Na Winfrida Mtoi Mechi ya Dabi ya Kariakoo ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara,...

Baraza la Mawaziri sasa Kidigital- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki...

SOMO KUTOKA KWA WATSWANA, WAFUATA NYAYO ZA WAZAMBIA KUING’ARISHA SADC

KUNA habari njema tena kutoka ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)....

More like this