Mashujaa wazitaka pointi tatu kwa Yanga

Na Winfrida Mtoi

Kueleke mchezo wao na Yanga, Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohammed Bares amesema wamejipanga kupata pointi tatu licha ya kwamba wanafahamu ugumu wa mechi hiyo.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utarajia kupigwa kesho Februari 8, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo uliopita timu hiyo ilifungwa na Simba bao 1-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani Lake Tanganyika, Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2024 jijini Dar es Salaam, Bares amesema wametoka kucheza mechi ngumu dhidi ya Simba wanaingia tena kwenye mechi ngumu lakini wamejipanga kuidhibiti Yanga.

“Ni mchezo mkubwa lakini kwenye mpira si mchezo mkubwa ni kujipanga tu na sisi tumejipanga kuidhibiti Yanga kwa sababu tunajua ina wachezaji wanaoweza kuamua matokeo,” amesema Bares.

Kwa upande wake mchezaji wa timu hiyo, Baraka Mtuwi amesema kwa kipindi hiki kila mchezo kwao wanacheza kama fainali na kuahidi kuwa hawatawaangusha mashabiki wao.

Mashujaa iliyoanza msimu huu kwa kasi hadi kukaa kwenye nafasi nne za juu mwanzoni mwa ligi hiyo, kwa sasa inashika nafasi ya 15 na alama tisa ikicheza michezo 13.

spot_img

Latest articles

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

Yanga yatua Zanzibar kuitengenezea dozi AS FAR Rabat

Na Winfrida Mtoi Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR...

Rais Samia atangaza Baraza Jipya la Mawaziri, nane watemwa

Tatu Mohamed na Winfrida Mtoi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,...

More like this