Tabianchi kikwazo uzalishaji mbegu

Na Faraja Masinde, Media Brains

Mabadiliko ya tabianchi imeelezwa kuwa moja ya changamoto inayoathiri sekta ya kilimo nchini hatua ambayo imesababisha hata mbegu zilizopo kushindwa kustahimili muda mrefu.

Moja ya athari za mabadiliko hayo ni pamoja na kuongezeka kwa joto linalosababisha mimea kushindwa kuhimili joto hilo, kuibuka kwa magonjwa mapya na wadudu wapya hali ambayo itawalazimisha watafiti hususan wa mbegu za mazao kufanya kazi ya ziada katika kubuni mbegu zinazoendana na mazingira ya sasa.

Changamoto hizo zinaibuka wakati ambapo Tanzania inatekeleza ajenda ya 10/30 inayolenga kuongeza mchango wa kilimo katika pato la taifa kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 ikiwamo kuwezesha vijana kuchangamkia kilimo kupitia mradi wa Jenga Kesho iliyobora (BBT).

Hayo yamebainishwa leo Novemba 4, 2023 mjini Bagamoyo mkoani Pwani na Mtaalamu na Mshauri wa Utafiti wa mbegu nchini, Dk. Emmarold Mneney, wakati wa warsha ya siku mbili ya kuwajengea uwezo Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kuhusu mbegu za mazao iyoandaliwa na Shirikisho la Uendelezaji na Ustawishaji wa Mifumo ya Chakula barani Afrika (AGRA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Media Brains.

Mwakilishi kutoka AGRA, Ipyana Mwakasaka akizungumzia jinsi taasisi hiyo ilivyojipanga kuwasaidia wakulima.

“Mabadiliko ya tabianchi sasa hivi yameingia kwenye kilimo na yameleta changamoto nyingi katika kupanda na kulima, kwa upande wa mbegu changamoto tunayoiona inatokana na mbegu tulizonazo za kisasa na za asili kwani hazikugunduliwa kukiwa kuna changamoto zilizopo sasa.

“Matatizo haya ni mapya na hizi mbegu tulizonazo haziwezi kustahimili, kwa hiyo kuna changamoto sasa ya watafiti wafanye ugunduzi wahakikishe kwamba hizi mbegu za asili au hizi tulizonazo sasa hivi zinapata hizi sifa za kukabiliana na mabadiliko haya ya tabianchi,” amesema Dk. Mneney.

Dk. Mneney amezitaja changamoto nyingi ambazo zinarudisha nyuma kilimo na upatikanaji wa mbegu kuwa ni pamoja na ukame wa muda mrefu nchini ikilinganishwa na miaka ya iliyopita.

“Changamoto kubwa hapa ni kuwapo kwa kipindi kirefu cha ukame hivyo mbegu zilizopo zinashindwa kustahimili muda huo bila maji, pia kuna ongezeko la joto ambalo mazao mengi yanashindwa kuhimili na hata yanayoota yanashindwa kutoa maua vizuri,” anasema Dk. Mneney.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Media Brains Ltd, Jesse Kwayu, akitoa neno katika mafunzo hayo.

Awali, akizungumza katika ufunguzi wa warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Media Brains Ltd, Jesse Kwayu amesema lengo la warsha hiyo ni kujenga uelewa wa kutosha kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini ambao wananafasi kubwa ya wakufaikia wananchi kupitia vyombo vyao.

“Tumeandaa warsha hii baada ya kuwapo kwa ufahamu mdogo kwa wananchi juu ya namna ya kupata mbegu bora jambo ambalo linarudisha nyuma azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa kilimo kinachangia asimilia 10 kwenye pato la Taifa ifikapo mwaka 2030.

“Mfano utaona kwa hapa nchini tafiti zinaonyesha kuwa hakuna zao lolote nchini ambalo mbegu zake zinazalishwa kwa walau asilimia 50, hakuna zote ni chini ya hapo iwe ni mahindi, maharage na mazao mengine,” amesema Kwayu.

Hali ya mbegu nchini

Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 20 tu ya wakulima nchini Tanzania ambao wanatumia mbegu bora hatua inayodhorotesha ufaisi wa kilimo.

Aidha, utafiti wa mahitaji ya mbegu unaonyesha kuwa mahitaji ya mbegu nchini Tanzania ni tani 120,000 hata hivyo kiwango hicho imekuwa ni changamoto kufikiwa, mathalani katika msimu wa kilimo wa 2020/21 mahitaji ya mbegu yalikuwa 97,928 huku upatikanaji wa mbegu ukiwa ni tani 85,005 tu sawa na upungufu wa tani 12,923.

spot_img

Latest articles

Balozi Nchimbi awafariji Mzee Makamba na Familia ya Mwambi

Na Mwandishi Wetu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea...

Mtanzania achaguliwa Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Dunia

Na Mwandishi Maalum, Washington D.C Benki ya Dunia imemchagua Mtanzania, Dk. Zarau  Kibwe, kuwa Mkurugenzi...

Shamba darasa kutoka Kenya: Hata Rais anatokwa jasho

KUNA kitu kinaitwa ‘shamba darasa’. Hili ni shamba ambalo huandaliwa na kuendeshwa kwa nia...

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi yaanza kazi, yakaribisha wananchi kutoa maoni

Na Winfrida Mtoi Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi nchini, imesema tayari imeanza...

More like this