Prof. Ndalichako: Mazingira mazuri ya uwekezaji yamechangia ukuaji wa muko wa NSSF

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako amesema mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa sekta binafsi yamechochea ukuaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Aidha, Prof. Ndalichako amesema ukuaji huo umepelekea thamani ya mfuko kuongezeka pamoja na michango ya wanachama.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo Agosti 17, 2023 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya NSSF kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii.

Amesema kwa mwaka 2022 mfuko huo uliandikisha wanachama 233,644 hadi kufikia Juni  mwaka 2023 kulikuwa na wanachama 243,895 na matarajio ifikapo Juni 2024 ni kuwa na wanachama 277,279.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, ameutaka mfuko wa NSSF kuhakikisha unaongeza wanachama zaidi hasa waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

Akijibu hoja za wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amewahakikishia wabunge kuzingatia maoni yao ili kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama wake.

spot_img

Latest articles

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

More like this