Balozi wa Tanzania UAE awasilisha Hati za Utambulisho

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo iliyopo Mjini Abu Dhabi.

Akizungumza baada ya kupokea hati hizo, Rais Al Nahyan alimuhakikishia, Balozi Mohamed ushirikiano na Serikali yake katika kutekeleza majukumu yake nchini UAE kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi Mohamed alimuahidi, Rais kuwa atahakikisha Watanzania na Waemirati wananufaika na fursa za kiuchumi zilizopo katika pande zote mbili.

Tanzania na UAE zina fursa nyingi za kushirikiana kiuchumi hususan katika sekta ya nishati ambayo UAE ni miongoni mwa nchi tajiri katika uzalishaji wa mafuta. Tanzania ina eneo kubwa la kilimo hivyo ina soko kubwa la bidhaa za Kilimo na Mifugo ambapo ushirikiano huo utawezesha uzalishaji wa kisasa na kuongeza thamani ya bidhaa.

Bidhaa zenye soko kubwa kwa Tanzania nchini UAE ni mbogamboga, matunda, nyama, korosho, karafuu, chai, karanga, asali, samaki na kahawa.

Pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu ubalozi huo pia unawakilisha nchi za Bahrain, Pakistan na Iran.

spot_img

Latest articles

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

Serikali: Tuchukue hatua kuepuka madhara ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA)

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia kwa Mkurugenzi msaidizi, Kitengo cha Afya Moja, Ofisi ya...

Serikali yawaita wadau kujitokeza kusapoti ushiriki wa wanawake michezoni

Na Winfrida Mtoi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' amewaomba...

More like this