Chongolo ‘kuhamia’ Dar

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, anatarajia kuhutubia katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Dar es Salaam Julai 29,2023 katika viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe.

Kufanyika kwa mkutano huo ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichokutana hivi karibuni jijini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kiliazimia katibu mkuu kufanya mikutano katika mikoa mbalimbali ukiwemo Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 25,2023 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abasi Mtemvu, amesema katika mkutano huo wataeleza utekekezaji wa Ilani ya Uchaguzi uliofanyika Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

“Dhamira ya CCM ni kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo, tunawaomba wananchi waje kwa wingi kwenye mkutano huu, tutaeleza utekelezaji wa Ilani na mambo mengi yanayoendelea nchini chini ya usimamizi wa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Mtemvu.

Chongolo anaendelea na ziara yake katika mikoa mbalimbali nchini ambapo tayari amefanya mikutano Mbeya, Mtwara, Lindi, Singida na Arusha.

spot_img

Latest articles

Vijana wahimizwa kuendelea kulinda amani

Na Tatu Mohamed VIJANA nchini wametakiwa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza amani iliyopo kwa kuwa wao...

Serikali ya Austria kufadhili miradi ya umeme Tanzania

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Austria kupitia Benki ya UniCredit imeahidi kuipatia fedha...

NIDA yawasajili watu wenye mahitaji maalum Temeke

Na Tatu Mohamed KATIKA kuadhimisha Siku ya Utambulisho Duniani, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)...

Mkurugenzi Mkuu Dawasa Mtaa kwa Mtaa kukagua huduma za maji

Na Mwandishi Wetu AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira...

More like this