Warning: Array to string conversion in /home/themedia/domains/themediabrains.com/public_html/wp-includes/shortcodes.php on line 434
Array

Balozi Dk. Shelukindo aiomba India kushirikiana na Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Media Barain

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo ameiomba Serikali ya India ishirikiane na Tanzania katika jitihada zake za kukuza sekta ya uchumi wa Buluu ambayo ni moja ya sekta ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita inayongoozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hayo wakati wa Mkutano wa 10 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano katika masuala ya uchumi, ufundi na sayansi kati ya Tanzania na India uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 26 Juni 2023.

“Napendekeza Serikali ya India ianzishe ushirikiano na Tanzania katika kuendeleza sekta ya uchumi wa buluu hususan, uvuvi kwenye bahari kuu, uendelezaji wa viwanda vya kusindika samaki, utafutaji na uokoaji, utengenezaji wa boat na vifaa vya kutengenezea boat,”, Balozi Shelukindo alisema.

Balozi Shelukindo aliitaja India kama Mshirika mkubwa na muhimu wa Tanzania katika sekta mbalimbali kama za biashara, uwekezaji, uendelezaji wa miundombinu, ulinzi, elimu na elimu ya ufundi. Alithibitisha hilo kwa kubainisha kuwa India ni nchi ya tatu kwa kufanya biashara na Tanzania, ambapo takwimu zilipo zinaonesha kuwa biashara kati ya nchi hizo mbili kwa mwaka 2021 – 2022 ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 6.

Aidha, Dk. Shelukindo alisema India ni moja ya nchi 5 zinazoongoza kwa uwekezaji nchini kwa kuwa na miradi yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.68, huku takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania zikionesha nchi hiyo kwa mwaka 2021 – 2022 imeandikisha miradi 630 iliyotoa ajira mpya zaidi ya 60,000.

Katibu Mkuu alitumia kikao hicho kuishukuru India kwa misaada mbalimbali inayoipatia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya maji. Alisema Serikali ya Tanzania inathamini mchango wa India kwa kutoa mikopo ya masharti nafuu ya Dola za Marekani Bilioni moja kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji nchini ambapo mwezi Juni 2022, kampuni sita zilisaini ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya Dola milioni 500 kwenye miji 28 itakayofaidisha zaidi ya watu milioni sita, ujenzi wake utakapokamilia.

spot_img

Latest articles

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...

Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini 📌 Apongeza utoaji wa mafunzo...

More like this

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...