Kinara wa kubebesha wanawake dawa za kulevya akamatwa

Na Esther Mnyika

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imemkamata kinara wa mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina ya cocaine nchini ambapo wanawake wanaongoza kubebeshwa dawa hizo kusafirisha maeneo mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa DCEA, Aretas Lyimo, mfanyabiashara huyo ana uwezo wa kusafirisha  watu 10 maarufu punda, huku wanawake wakiongoza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 25,2024 jijini Dar es Salaam, Lyimo amesema mfanyabiashara huyo aliyekuwa anatafutwa tangu mwaka 2000, amekamatwa maeneo ya Boko jijini humo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 25,2024, jijini Dar es Salaam.

Amesema wamefanikiwa kumkamata akiwa na  gramu 692.336  kutokana na oparesheni inayoendelea  nchinj kwa sasa.
 
“Mfanyabiashara huyu wa mtandao wa cocaine  ambaye alikuwa anatafutwa mda mrefu  kabla ofisi ya DCEA haijafunguliwa ni miaka 23  anatafutwa hivyo alikamatwa katika  eneo la Boko Wilaya ya Kinondoni  pamoja na washirika wake watatu,”amesema Kamishna Lyimo.

Ameeleza kuwa  kati yao wawili walikamatwa jijini Dar es Salaam  na mmoja amekamatwa katika Kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini.

Amesema wasafirishaji huwa wanazimeza zikiwa katika mfumo  wa pipi ambapo kwa mara moja mtu anabeba  kuanzia gramu 300 hadi 1200 na wengine  hadi gramu 2000 kwa wakati mmoja.

Aidha ametangaza oparesheni kali ya dawa za kulevya ya 2024 ambayo itafanyika nchi kavu na baharini katika kumbi za starehe,hoteli za watumia shisha.

Amefafanua kuwa  oparesheni ya nchi kavu itahusisha mashamba ya dawa za kulevya kwenye mipaka na maeneo ya mjini kwa upande wa bahari zitahusisha fukwe na katikati ya bahari.

spot_img

Latest articles

SMZ yapongeza udhamini mnono wa NMB Mapinduzi Cup

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeipongeza Benki ya NMB kwa...

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

More like this

SMZ yapongeza udhamini mnono wa NMB Mapinduzi Cup

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeipongeza Benki ya NMB kwa...

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...