Jeshi la Polisi lachunguza  taarifa ya OCD  Chunya

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi limesema limeona na linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya (OCD), mkoani Mbeya kwa waandishi wa habari kama ushauri kwa wamiliki wa vituo vya mafuta wilayani humo.

Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Jeshi hilo leo Novemba 26,2025, imesema uchunguzi unafanyika ili kupata ukweli wa taarifa hiyo, kwani hana mamlaka ya kuita waandishi wa habari na kutoa taarifa kwao. “Ikibainika hivyo hatua stahiki zitachukuliwa mara moja.

Mapema leo ilisambaa video ikimuonesha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya (OCD), akitoa angalizo kwa wauzaji wa mafuta katika Wilaya hiyo, pamoja na kuwataka wasiwauzie madereva wa bodaboda mafuta yanayozidi lita mbili kwa wakati mmoja kuelekea Desemba 9, 2025.

spot_img

Latest articles

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

More like this

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...