Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, kutokana na sababu za kiusalama.

Leo Novemba 10, 2025 Lissu alitarajiwa kufikishwa  katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, wakisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, kwa ajili ya kusikilizwa kwa shahidi wa nne wa upande wa Jamhuri kutoa ushahidi wake dhidi ya kiongozi huyo wa Chadema.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Thawabu Issa, aliieleza mahakama kuwa walifika mahakamani na  kugundua kwamba mshtakiwa hakuwepo, hivyo kufanya  jitihada za kuwasiliana na Mkuu wa Gereza kujua sababu za kutokuwepo kwake.

“Tulipofika hapa tulikuta mshtakiwa hayupo. Tulifanya jitihada za kuwasiliana na Mkuu wa Gereza na tukaelezwa kwamba wameshindwa kumfikisha kwa sababu za kiusalama,” amesema Wakili Issa.

Upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama kuhairisha kesi hiyo kwa siku 14, lakini katika maamuzi yake Mahakama kupitia Jaji Danstan Ndunguru ikatoa maelekezo kuwa shauri hilo linaahirishwa hadi Jumatano na si kwa siku 14 kama ilivyoombwa na Jamhuri. Huku akisisitiza  kuwa mshtakiwa  pamoja na wafikishwe makahamani ili shauri liendelee.

spot_img

Latest articles

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

More like this

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...