Na Mwandishi Wetu
Askofu Mkuu Wapo Mission, Dk. Sylvester Gamanywa

“Mungu ambaye tunamwakilisha ndiye anayweka watawala na ndiye anayewaondoa watawala, kwa kutumia mifumo ambayo ni halali na kisheria katika Mataifa yetu. Tanzania pia ni miongoni mwa nchi ambazo Mwenyezi Mungu ametupa utawala kwa awamu sita na imani yangu tarehe 29, Mwenyezi Mungu ambaye tumemuomba anakwenda kutupa mtawala ambaye amekwisha kumteua na kumthibitisha baada ya zoezi la uchaguzi mkuu kufanyika kwa amani na utulivu. Sina mashaka Mungu ambaye ni mkuu atadhibiti na atatushangaza,”
Sheikh Twalib Ahmed

“Tunatoa angalizo na kuwakumbusha ndugu zetu wote wakataochaguliwa katika vyeo mbalimbali, hilo ni jukumu Mwenyezi Mungu ameliweka wewe, ukalibeba kwa hivyo litekeleze kwa uaminifu, kwa huruma, kwa upole. Na kitu kikubwa zaidi, wanyonge. Ukiwa kiongozi basi lazima ujue wew sio Bwana, ukiwa kiongozi wewe ni mtumishi lazima ufikishe haki kwa wenyewe. Kwa hiyo tunatarajia Mwenyezi Mungu atatufikisha katika eneo hilo na nchi yetu ni kisiwa cha amani tuidumishe amani,”
Katibu Mkuu wa JMAT, Dk. Ole Gabriel Maasa

“Biblia inasema hivi: Yusufu alifunga safari kutoka Nazareti akaenda Bethelehemu kwenda kujiandikisha kupiga kura. Biblia inatuonesha uhalali wa kupiga kura. Kumzuia mtanzania kutimiza haki yake ya kupiga kura ni kwenda kinyumbe na Biblia takatifu, Watanzania wote tujitokezeke, tutumie haki yetu kupiga kura na baada ya kupiga kura tubaki na amani yetu.
Sheikh Rajabu Katimba (Almalid)

“Amani ni ibada, anatakayevunja amani si anatukosea sisi tu, anamkusea Mwenyezi Mungu. Nakata niombe ndugu zangu waislamu na wasio waislamu, jamaa zetu wote kulinda amani ya nchi ili tuzidi kuwepo kwa ajili ya kufanya ibada na Mwenyezi Mungu ajaalie katika hili tupite kwa amani na salama.
Murtaza Adam Jee Jamii ya Bohora Tanzania

“Amani inaanza moyoni, mioyo yeti inaongozwa na Imani. Sisi kama viongozi wa dini tuna fursa kubwa wakati tunakwenda kuongea na waumini wetu kuwagusa mioyo yao iridhike kuhusu kuweka nchi yao mbele. Watu wana mitazamo mbalimbali lakini tukiweka Tanzania mbele mioyo itaridhika.
Askofu Janeth Mabondo

“Sisi kama watoto wa baba mmoja, mama mmoja Tanzania, uchaguzi ukikamilika, huyo baba ambaye atatupa au mama atatupa, basi amani ya watu wote itakuwa nzuri, tushikamane pamoja hata kama siasa ilienda sivyo au ndivyo”, amesema.


