Rais Samia awapiga chini mabosi Mwendokasi

Na Mwandishi Wetu, The Media Brains

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa mabosi wapya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) maarufu Mwendokasi   kwa kuwaondoa Mtendaji  Mkuu Dk. Athuman Kihamia na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni UDART, Waziri Kindamba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga, walioteuliwa ni Said Tunda anayechukua nafasi ya Dk. Kihamia na  Pius Ng’ingo anayechukua nafasi ya Waziri Kindamba.

Uteuzi huo unakuja siku moja baada ya wananchi kufanya fujo kwa kupiga mawe mabasi hayo jana katika maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam kutokana na kuchoshwa na hali ya usafiri  huo.

Wakati uteuzi huo unafanyika tayari mabasi mapya yameanza kufanya kazi katika njia  ya Kimara, Gerezani,  Kivukoni na Morocco.

spot_img

Latest articles

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

Serikali yaahidi kuimarisha uwezeshaji wa Makundi Maalum kupitia ajenda ya Maendeleo Jumuishi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt....

More like this