Huduma ya Maji Dar na Pwani yaimarika

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya majisafi ndani ya eneo lake la kihuduma na kuendelea kupita mtaani kujiridhisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa Wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro ametembelea wateja katika Wilaya za Ubungo na Ilala na kujionea uimarikaji wa huduma za Maji na kusema kuwa lengo la DAWASA ni kuhakikisha kila Mwananchi anapata huduma ya Maji.

“Leo tumetembea na kuona hali ya huduma kuimarika na kwa msukumo mkubwa na sehemu nyingine huduma inaendelea kutengamaakidogo kidogo, kwa maeneo tuliyotembelea kama kwa wakazi wa Wilaya za Ubungo na Ilala katika mitaa ya Kilungule A & B, Korogwe, Ziimbili, Ulongoni A, Mongo la ndege, Kichangani, Kinyerezi, Buguruni Kisiwani, mtaa wa Ghana na Malapa hali ya huduma inaridhisha,” amesema Everlasting.

Kwa upande wake , mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule A, Kaini Kyejo ameipongeza jitihada za haraka zilizofanyika na Mamlaka katika kurejesha huduma ya maji ambayo ni tegemeo la msingi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kila siku majumbani.

“Wananchi wangu tayari wameanza kupata huduma ya maji na nimewatembelea lakini sio wote yanatoka kwa msukumo mkubwa lakini wamenihakikishia ni swala la muda kwa kuwa huduma inamairika,” amesema Kyejo.

Mkazi wa Mbezi Msakuzi, Alice Makamba amesema huduma ya maji kwa kipindi cha siku mbili haikuwepo lakini walipata taarifa za maboresho yanayoendelea katika Mtambo wa Ruvu juu na kwa sasa huduma imerejea na imeendelea kuimarika.

“Kwa kweli kipindi cha siku mbili huduma hatukuwa nayo lakini tulipewa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna matengezo huko Ruvu Juu na huduma imerejea japo kwa msukumo haujaimarika sana ila maji tunapata,” amesema Alice.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

More like this