Watumishi Wizara ya Nishati wapatiwa elimu ya matumizi sahihi ya Nishati Safi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu

WATUMISHI wa Wizara ya Nishati leo wamepata elimu ya matumizi bora na sahihi ya majiko yanayotumia umeme kidogo ( Induction cookers) baada ya kukabidhiwa majiko hayo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko hivi karibuni.

Dkt. Biteko aliwakabidhi majiko hayo Watumishi wa Wizara ya Nishati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kwa kutambua kuwa Watumishi hao ni mabalozi katika utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa wananchi.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati- Mtumba, Dodoma yameandaliwa na Kitengo cha Nishati safi ya kupikia kwa kushirikiana na wataalam kutoka Kampuni ya Positive Cooker.

Akitoa elimu ya matumizi bora na sahihi ya majiko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Positive Cooker, Atukuzwe Willson ameeleza kuwa lengo la utoaji wa mafunzo hayo ni sehemu ya uhamasishaji wananchi kutumia umeme kwa matumizi ya kupikia kupitia majiko janja yanayotumia umeme kidogo.

“Lengo la kutoa elimu hii ni kuhakikisha kila Mtanzania anaachana na matumizi ya nishati isiyosafi ili kulinda mazingira pamoja na afya zetu lakini pia ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono kampeni ya nishati safi ya kupikia ambapo hadi kufikia mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanapaswa kutumia nishati safi ya kupikia,” amesema Willson.

Akizungumza kuhusu majiko hayo janja ya umeme amesema yanatumia wastani wa nusu uniti hadi uniti moja na nusu kwa wastani wa dakika 15 mpaka dakika 90 sawa na shilingi 65 mpaka shilingi 534 tu hali inayothibitisha ufanisi wa majiko hayo kuwa na gharama nafuu, kuokoa muda, kulinda afya pamoja na mazingira.

spot_img

Latest articles

Fahad Soud ajinyakulia IST kupitia Simbanking ya CRDB

Na Mwandishi Wetu MKAZI wa Jiji la Tanga, Fahad Soud, ameibuka mshindi wa pili wa...

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waridhishwa na kasi ya utekelezaji Bwawa la Kidunda

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wametembelea mradi wa ujenzi wa...

Ukatili huu wa Polisi unawapa faraja gani?

UKATILI uliofanywa na baadhi ya askari polisi dhidi ya raia waliokuwa wanakwenda kusikiliza kesi...

Mwendokasi: Adha kwa abiria, gubu la madereva

Na Mwandishi Wetu Inakaribia miaka 10 tangu usafiri wa mabasi ya haraka maarufu kama Mwendokasi...

More like this