Mkurugenzi Mkuu Dawasa Mtaa kwa Mtaa kukagua huduma za maji

Na Mwandishi Wetu

AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amefanya ziara ya kikazi kukagua hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya Ubungo, Mburahati, Magomeni, Saranga na Kinyerezi.

Ziara hiyo ililenga kujionea hali halisi ya upatikanaji wa maji na kutafuta suluhisho katika maeneo yenye changamoto za kihuduma zinazowakabili wananchi.

“Huduma ya Maji katika eneo letu la kihuduma Dar na Pwani iko vizuri na leo tunapita mitaani kukagua na kujiridhisha upatikanaji wa huduma tunayozalisha kama inawafikia wananchi na iwapo kama kuna changamoto basi tunazitatua na wananchi wanaendelea kufurahia huduma” amesema Mhandisi Bwire.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyerezi, Hassan Hamiss Nandeta, ameishukuru DAWASA kwa hatua madhubuti ilizochukua katika kuboresha huduma ya maji safi kwenye maeneo yao, akibainisha kuwa wananchi wameanza kunufaika na maboresho hayo.

DAWASA inaendelea kutekeleza mkakati wa kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo jirani, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora na ya uhakika.

spot_img

Latest articles

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

More like this

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...