CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wamezindua rasmi programu ya Ajira Ye2 itakayowawezesha vijana na wanawake zaidi ya 500 kupata ajira na kukuza biashara zao kupitia mafunzo, mitaji na ushauri wa kitaalamu.

Akizungumza leo Septemba 16, 2025 wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa CRDB Foundation, Tully Esther Mwambapa, amesema programu hiyo inalenga kuwajengea uwezo wajasiriamali kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Zanzibar ili kukuza biashara na kuongeza nafasi za ajira.

“Wanufaika wa mradi huu watajengewa uwezo wa kielimu kuhusu masoko, fedha, usimamizi wa biashara na jinsi ya kutafuta fursa kidigitali. Pia watapatiwa ushauri wa kitaalamu kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka kwa wabia wetu mbalimbali wakiwemo SIDO, VETA, NIT, TRA, BRELA, TBS, WMA na TWCC,” amesema Tully.

Aidha, ameongeza kuwa washiriki pia wataunganishwa na wawekezaji kupitia maonesho mbalimbali ya kibiashara, huku watakaohitimu na kukidhi vigezo wakipata fursa ya kupewa mtaji wezeshi hadi Sh milioni 200 kupitia programu ya Imbeju.

Kwa mujibu wake, zaidi ya Sh bilioni 3 zimetengwa ili kuwawezesha wanawake na vijana kupitia mradi huo, ambao vipaumbele vyake vitakuwa tofauti kulingana na kila mkoa.

Ametaja kwa Mkoa wa Dar es Salaam kipaumbele ni katika Nishati mbadala, usimamizi na udhibiti wa taka, viwanda vidogo rafiki kwa mazingira na uchumi wa buluu, Morogoro imelenga kilimo hai, usindikaji na ufungashaji, huku Zanzibar ikilenga uchumi wa buluu, bidhaa za asili hasa viungo na vipodozi, pamoja na utalii wa kimazingira.

Tully ametoa wito kwa wanaohitaji kushiriki, kuwasilisha maombi yao kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 16, 2025 kupitia tovuti ya CRDB Bank Foundation na mitandao yote ya kijamii ya CRDB.

Kwa upande wake, mwakilishi wa GIZ, Dennis Mbangulla, amesema wanafurahishwa na ushirikiano huo na wanaamini utazalisha matokeo makubwa.

“Tumeendelea kushirikiana na CRDB kwenye miradi mbalimbali, na kupitia mradi huu wa Ajira Yetu tunatarajia kuzalisha ajira nyingi zaidi. Ushirikiano huu utafungua milango ya kutekeleza miradi mingine kwa pamoja ikiwemo afya, maji na maendeleo ya jamii,” amesema Mbangulla.

spot_img

Latest articles

Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma 650...

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...

More like this

Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma 650...

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...