Mvua za vuli kunyesha kwa wastani  kuanzia  Oktoba

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa msimu wa mvua za vuli kwa mwaka 2025, unaotarajiwa kuanzia Oktoba hadi Desemba, utakuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya nchi.

Msimu huo utatawaliwa na vipindi virefu vya ukavu pamoja na mtawanyiko usioridhisha wa mvua, hasa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Ladislaus Chang’a, wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Oktoba 2025 katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Amesema kuwa mvua hizo zitaendelea kusambaa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki kuanzia wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Novemba 2025.

“Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari 2026, mvua za vuli zinatarajiwa kuongezeka kidogo mwezi Desemba 2025, huku vipindi vya joto kali kuliko kawaida vikitarajiwa kutokea katika msimu huo”Amesema Chang’a

Aidha Dk. Chang’a ametoa wito kwa wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za hali ya hewa zinazotolewa na TMA, zikiwemo utabiri wa saa 24, siku 10, na mwezi mmoja, pamoja na tahadhari zinazotolewa mara kwa mara.

Ameeleza kuwa mwelekeo huo wa msimu ni wa muda wa miezi mitatu, hivyo mabadiliko ya muda mfupi na mwenendo wa mifumo ya mvua yataendelea kufuatiliwa na kuwasilishwa kwa wakati.

spot_img

Latest articles

Tembo Warriors yatinga nusu fainali CECAAF

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu Tanzania 'Tembo Warriors' imefanikiwa kutinga...

Ajali yaua wanafunzi wawili wa kidato cha sita

Na Mwandishi Wetu Watu saba wamefariki dunia wakiwamo wanafunzi wawili wa kidato cha sita shule...

Mpina ashinda kesi, ruksa kugombea Urais

Na Mwandishi Wetu Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina leo Septemba...

Mahakama kuamua hatma ya Lissu Jumatatu

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Tundu Lissu,  amerejeshwa...

More like this