Na Mwandishi Wetu
Watu saba wamefariki dunia wakiwamo wanafunzi wawili wa kidato cha sita shule ya Sekondari Songe, Musoma baada ya gari aina ya Toyota Succeed walilokuwa wakisafiria kugonga kwa nyuma Fuso lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kuharibika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Mark Njera, ajali hiyo imetokea Kijiji cha Buganjo wilayani Rorya leo Septemba 11,2025 saa 11 alfajiri.
Amewataja wanafunzi hao kuwa ni Kwinta Gerald(18) Anitha Selemani(18). Wengine waliofariki ni Kelivin Orando(28), Ombura Ududo(34), John Abraham(30), Sharome Benard(30) wote wakazi wa Rorya.

Kamanda Njera amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni ni mwendokasi wa dereva wa gari aina ya Toyota Succeed kwa kuendesha bila kuchukua tahadhari.
Ameeleza kuwa dereva wa gari aina ya Mitsubish Fuso iliyokuwa imeharibika na kupaki pembeni mwa barabara ilichukua tahadhari kwa kuweka alama(reflective triangle).