Mradi wa TACTICS waleta mageuzi ya miundombinu Morogoro

Na Mwandishi Wetu

MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuboresha miundombinu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro hasa baada ya ujenzi wa barabara na mitaro ya maji ya mvua.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo ambapo ameeleza kuwa miradi ya ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua pamoja na barabara imefikia asilimia 95 kukamilika.

“Kuna maeneo ya makazi ya watu ambapo kipindi cha mvua yalijaa maji nakusababisha kero kwa wananchi lakini kukamilika kwa ujenzi wa mitaro sasa maji hayatuami na kero imeondoka pia thamani ya maeneo kama viwanja na nyumba imepanda baada ya maeneo mengi kuanza kufikika kwa urahisi”, amesema.

Aidha, Rose Munisi ambaye alikuwa mhanga wa mafuriko kipindi cha masika ameipongeza Serikali kwa kuchukua hatua hiyo muhimu ya ujenzi wa mifereji ya maji na kuongeza kuwa watahakikisha miundombinu hiyo inalindwa.

“Sisi wenyewe ni walinzi wa miundombinu hii na hatutakubali kuona mtu anatupa taka kwenye mitaro maana hapo awali tulipata tabu kweli kipindi cha mvua”, amesema Rose.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kihonda, Tatu Khamis amesema kuwa ujenzi wa barabara katika kata hiyo umekuwa kiunganishi na stendi ya Treni ya Mwendokasi (SGR) na kusema kuwa licha ya kupendezesha maeneo hayo pia barabara itakuza uchumi wa wananchi.

Kwa upande wake, Mohamed Ramadhani ambaye ni Mkazi wa Tungi amesema kuwa hapo mwanzo kabla ya ujenzi wa barabara hali ilikuwa mbaya ambapo watoto kwenda shule na hata hospitalini ilikuwa ni changamoto hasa wakati wa masika ila kwa sasa wanaweza kufanya kazi zao na kusafiri bila shida kutokana na uwepo wa barabara.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this