Mfanyabiashara wa nguo ajinyakulia Gari ya IST kupitia SimBanking ya CRDB

Na Mwandishi Wetu

MKAZI wa Tabata jijini Dar es Salaam, Said Mbaruku, ameibuka mshindi wa gari jipya aina ya IST kupitia kampeni ya kipekee ya Benki ya CRDB inayolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali, hususan SimBanking.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo iliyofanyika jana Tabata Segerea , Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi kutoka CRDB, Steven Adili, alisema kampeni hiyo inalenga kurudisha fadhila kwa wateja wao wanaotumia huduma za benki hiyo kwa njia ya kidijitali. 

Alieleza kuwa mbali na magari aina ya IST yanayotolewa kila mwezi, kuna zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo fedha taslimu zaidi ya Sh milioni 200 zinazotolewa kila siku.

“Ili kuingia kwenye droo, ni lazima uwe na akaunti ya CRDB na umejiunga na huduma ya SimBanking. Kila muamala unaoufanya, kama vile kununua umeme, kulipia bili, au kukata tiketi za SGR, unakupa nafasi ya kushinda,” alisema Adili.

Kwa mujibu wa CRDB, droo hiyo itaendelea hadi mwezi Disemba ambapo mshindi wa mwisho atajishindia gari aina ya Harrier Anaconda.

“Tunahamasisha wananchi wote kutumia SimBanking. Huduma hii haijabagua ni kwa wanafunzi, wafanyabiashara, wafanyakazi binafsi na hata watumishi wa umma,” aliongeza Adili.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni tanzu ya CRDB Insurance, Wilson Mzanva alisema kuwa gari lililokabidhiwa mshindi huyo limewekewa mafuta full tank kama sehemu ya kuonesha thamani ya wateja wa benki hiyo.

“CRDB inatoa huduma zake kupitia matawi zaidi ya 260 pamoja na mawakala zaidi ya 25,000 nchi nzima. Kwa sasa, huduma za SimBanking zinapatikana hata kwa wale wasio na smartphone kupitia USSD (*150*03#), pamoja na kupitia app rasmi ya SimBanking,” alisema.

Said Mbaruku, ambaye ni mfanyabiashara wa duka la nguo, alielezea furaha yake baada ya kupokea taarifa za ushindi wake. 

“Nilishangaa sana nilivyopokea SMS kuwa nimeshinda, lakini nilianza kuamini baada ya kupigiwa simu. Sikutarajia kabisa, nilishinda kwa kununua umeme wa Sh 10,000 tu kupitia SimBanking.”

spot_img

Latest articles

JAB yawafungia watangazaji wanne wa kipindi cha Genge la GEN TOK kwa kukiuka maadili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewafungia...

Madai ya dada wa Polepole kubebwa, Polisi yachunguza 

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limesema limepokea taarifa za...

Kiungo Moussa  Conte rasmi atambulishwa Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania, Klabu ya Yanga...

Tanzania kuwa na mashirika ya umma yenye ushindani ifikapo 2050

Na Mwandishi Wetu IFIKAPO mwaka 2050, Tanzania inajiona kuwa na Mashirika ya umma ya...

More like this

JAB yawafungia watangazaji wanne wa kipindi cha Genge la GEN TOK kwa kukiuka maadili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewafungia...

Madai ya dada wa Polepole kubebwa, Polisi yachunguza 

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limesema limepokea taarifa za...

Kiungo Moussa  Conte rasmi atambulishwa Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania, Klabu ya Yanga...