Waziri Chana akutana na Sekretarieti ya Mkataba wa Lusaka

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya mkataba wa Lusaka (Lusaka Agreement) kuhusu Mkutano wa 14 wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka(LATF) unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Mei 6-8, 2025.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma leo Aprili 30, 2025, amesema Tanzania iko tayari kupokea wageni zaidi ya 100 kutoka Nchi wanachama na Nchi waalikwa na kuwahakikishia usalama wao kwa kipindi chote wawapo nchini.

Naye, Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Mkataba wa Lusaka, Edward Phiri amesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na tayari viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka wameshathibitisha kushiriki.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia maliasili), CP Benedict Wakulyamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia utalii), Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Alexander Lobora pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this