Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco afariki dunia kwa ajali

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO) Gissima Nyamo-Hanga amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025 kwa ajali iliyotokea Wilayani Bunda mkoani Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Evansi Mtambi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amefafanua kuwa tukio limetokea kati ya saa 6 hadi 7 usiku wa kuamkia leo.

“Ni kweli tukio lipo na Gissima amefariki Dunia na RPC atakuwa na taarifa kwa kina,” amesema Mtambi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidia kutoa taarifa kwa kina badae kidogo.

Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara Nicksoni Babu amebainisha kuwa Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule Wilaya ya Bunda huku wakisubiria taarifa zaidi na taratibu nyingine.

Media Brains inatoa pole kwa Menejimeti ya Tanesco ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

More like this