EWURA yatangaza bei za Mafuta kwa mwezi Aprili 2025

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi Aprili, zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 02 Aprili 2025 saa 6:01 usiku.

Kwa mwezi huu, gharama za uagizaji mafuta (premiums) zimepungua kwa wastani wa asilimia 6.08 kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.09 kwa mafuta dizeli na kuongezeka kwa asilimia 1.11 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam, huku bandari ya Tanga kukiwa hakuna mabadiliko, na kwa bandari ya Mtwara zimepungua kwa wastani wa asilimia 4.00 kwa mafuta ya petroli na dizeli.

Katika bei kikomo kwa mwezi Aprili 2025, bei za mafuta katika soko la dunia zimepungua kwa asilimia 6.92 ya kwa mafuta ya petroli, asilimia 6.57 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 7.82 kwa mafuta ya taa mtawalia. Bei zinazozingatiwa za mafuta yaliyosafishwa (FOB) ni za soko la Uarabuni.

Kwa bei za mwezi Aprili 2025, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umeongezeka kwa asilimia 1.91.huku

EWURA imewakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa na atua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayekiuka agizo hilo.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this