ETDCO wakamilisha mradi wa Kilovoti 132 Tabora-Urambo

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme ( ETDCO) imefanikiwa kuwasha rasmi laini ya msongo wa Kilovolti 132 yenye mrefu wa kilomita 115 kutoka Tabora hadi Urambo ambao unakwenda kuwasaidia wananchi wa Urambo na Kaliua kupata umeme wa uhakika na kuchochea maendeleo.

Akizungumza Machi 20, 2025 mkoani Tabora katika zoezi la kuwasha laini hiyo mpya ya Tabora hadi Urambo, Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya ETDCO CPA. Sadock Mugendi, ameishukuru Serikali pamoja na Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kwa kuwaamini kutekeleza mradi huo, huku akieleza kuwa wananchi wa Wilaya ya Urambo na Kaliua wategemee kupata umeme wa uhakika.

CPA. Mugendi amesema kuwa mradi huo umetekelezwa na watalaamu wazawa jambo ambalo limeonesha wanaweze kutekeleza miradi ya umeme kwa wakati bila tatizo lolote.

Meneja wa Mradi wa Tabora- Katavi kwa upande wa TANESCO Mhandisi Sospeter Oralo, amesema kuwa mradi huu umegharimu shilingi billioni 40, ambapo gharama ya laini yenye msongo wa Kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Urambo ni bilioni 24, huku ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Urambo zimetumika bilioni 16 fedha ambazo zimetoka serikali ya Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Ufundi ETDCO Mhadisi Dismas Massawe, amesema kuwa baada ya kuwasha laini hiyo wananchi wa Urambo na Kaliua watarajie kupata umeme wa uhakika kupitia kituo cha Uhuru Wilaya urambo chenye mashine umba (transformer) ya Megawatts 28.

Naye, Meneja wa Mradi wa Tabora hadi Urambo upande wa ETDCO Mhandisi Ntuli Burton, amesema kuwa mradi huu ulianza April 2024 na tulitegemea kumalizika June 2025.

“Tunashukuru Mungu tumefanikiwa kumaliza mradi huu kabla ya wakati ili wananchi wa Urambo waweze kupata umeme wa uhakika haraka iwezekanavyo,” amesema.

Kupitia mradi huo wa kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Urambo wenye msongo wa kilovolti 132 utasiadia kuchochea maendeleo katika Wilaya ya Urambo, Kaliua pamoja na Mkoa wa Tabora kwa ujumla.

spot_img

Latest articles

DAWASA YAREJESHA MAJI KIKONGO BAADA YA MIAKA MIWILI

Na Mwandishi Wetu WAKAZI takribani 1,500 wa Vijiji vya Lupunga, Videte na Kwa Mkino,...

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...

More like this

DAWASA YAREJESHA MAJI KIKONGO BAADA YA MIAKA MIWILI

Na Mwandishi Wetu WAKAZI takribani 1,500 wa Vijiji vya Lupunga, Videte na Kwa Mkino,...

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta...