Rais Mwinyi azindua Kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Uwekezaji wa Kituo cha Kisasa cha Ukaguzi na Upasishaji wa Vyombo vya Moto ni Mapinduzi Makubwa katika Sekta ya Usafiri hapa Nchini.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza katika Ufunguzi wa kituo hicho Kwasilva kiliopo Dole Kizimbani Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kituo hicho ambacho ni Ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Kizalendo ya Zenj General Mechandize kina Uwezo wa kuhudumia Vyombo vya moto Takribani 300 kwa Siku kwa kutumia mashine na Teknolojia ya Ukaguzi yenye Viwango vya Kimataifa.

Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kituo hicho ni muhimu kwa Ukuaji na Maendeleo ya Sekta ya Usafiri na kitafungua Ukurasa Mpya wa Usalama wa Usafiri Barabarani.

Pia Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuthamini na kushirikiana na Sekta binafsi kufanikisha miradi ya Uwekezaji ya ndani na ile inayotoka nje ya nchi kwa mafanikio makubwa.

Akizungumzia Usafiri wa Umma Dkt.Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuwa na Usafiri wa Mabasi ya Kisasa ya Umeme yatakayotoa huduma Bora kwa Wananchi.

Akiwasilisha Taarifa ya Kitaalamu ya Mradi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi Habiba Hassan amesema Mradi huo wa Ubia baina ya Kampuni ya Zenj General Mechandise na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umegharimu Shillingi Bilioni 2.8 hadi kukamilika kwake na una Uwezo wa kukagua Vyombo vya Moto 300 kwa siku.

spot_img

Latest articles

WAZIRI MKUU ASISITIZA AFRIKA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA USAFIRI WA MAJINI

Na Tatu Mohamed WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano...

NDEJEMBI: MRADI WA TAZA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA KIUCHUMI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

📍 Akagua maendeleo ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme TAZA Sumbawanga na Songwe 📍...

Askofu Malasusa: Prof. Mmari alikuwa mnyenyekevu, mcha Mungu

Na Winfrida Mtoi Mkuu wa Kanisa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk....

TANESCO KUONGEZA UWEZO WA UPATIKANAJI WA UMEME KATAVI DISEMBA 1,2026-MD TWANGE

📌Aeleza Mpanda itakuwa na jumla ya megawati 80 na kukidhi mahitaji ya juu ya...

More like this