WAZIRI HOMERA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUONGOZA KWA VITENDO AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA BARANI AFRIKA

📌Ataja matumizi ya nishati safi kupanda kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 28.6 mwaka 2025

📌Wizara kuja na mkakati kabambe wa kuwawezesha vijana kutengeneza majiko banifu nchi nzima

📌TANESCO, REA na TPDC kuongeza kasi ya utoaji elimu na usambazaji wa majiko banifu na ya umeme

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nishati, Juma Homera, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuongoza jitihada za kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, akisema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza ajenda hiyo barani Afrika.

Waziri Homera alitoa pongezi hizo Novemba 11, 2026 wakati akitoa salamu za ukaribisho za Wizara ya Nishati kwa Rais Samia katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kutangaza mafanikio ya mpito wa Nishati Tanzania na Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Shule na Vituo vya Afya, uliofanyika pembezoni mwa COP31 jijini Antalya, Türkiye.

Alieleza kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini yameongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 28.6 mwaka 2025, hatua inayoonesha maendeleo katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa 2024–2034.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo na taasisi za kimataifa kujadili mafanikio, fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano katika kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Tanzania inalenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

spot_img

Latest articles

HAKIKISHENI MNAMBANA MKANDARASI ILI MRADI WA UMEME SONGEA – MASASI UKAMILIKE KWA WAKATI – MHE. NDEJEMBI

📌Akagua Mradi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa Kv 220 Songea...

WATALII HIFADHI ZA TAIFA WAFIKIA MILIONI 1.5

Na Tatu Mohamed  IDADI ya watalii waliotembelea hifadhi za taifa nchini imeongezeka kutoka watalii 768,319...

OTR na TAZAMA zajadili mwelekeo wa biashara

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) na Kampuni ya Bomba la Mafuta...

MATENGENEZO YA BOMBA MPIJI YAKAMILIKA, DAWASA YAINGIA MTAANI

Na Mwandishi Wetu HUDUMA ya maji imeanza kurejea katika maeneo mbalimbali ya Dar es...

More like this