Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wa Dk. James Andilile Mwainyekule.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyotolewa leo Aprili 2, 2026, Dk. Mwaiyukule atapangiwa majukumu mengine.

Utenguzi huo umekuja siku moja baada ya jana Aprili Mosi, 2026, EWURA kutangaza kupanda kwa bei petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Katika hatua nyingine Rais Samia amefanya uteuzi, uhamisho, ambapo Prof. Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu). kabla ya uteuzi huo Mhe. alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu (Kazi Maalum).

Reuben Kwagilwa amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Dk.Festo Dugange amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Masuala ya Elimu;

Naye Balozi Ali Jabir Mwadini ameteuliwa kuwa Katibu wa Rais, wakati Dk. Eveline Munisi ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Rais Samia amemteua Angela Kizigha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Balozi Said Othman Yakub amepangiwa kuwa Balozi wa wa Tanzania nchini Ufaransa.

spot_img

Latest articles

Nishati Safi yafungua milango ya fursa kwa watengeneza maudhui

Na Mwandishi Wetu, Mwanza WATENGENEZA maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa...

WARAKA WA MWANDOSYA KUMBUKUMBU YA MWAPACHU

KUMKUMBUKA MAREHEMU BALOZI JUMA VOLTER MWAPACHU Balozi Juma Volter Mwapachu (Mwenyezi Mungu Amrehemu), mwanasheria, mwanadiplomasia,...

Bajeti za Mashirika ya Umma kuchambuliwa kuakisi Dira 2050

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) imeanza zoezi la uchambuzi wa mipango...

CAG Kichere kama Prof. Assad anakubali Bunge ni dhaifu?

JUMATATU wiki hii taifa lilishuhudia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

More like this