Lukuvi afariki dunia

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi (70) amefariki dunia saa 1:00 asubuhi ya leo Jumatano, Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kifo hicho kimetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka juu ya msiba huo wa Lukuvi aliyezaliwa Agosti 15, 1955.

Taarifa hiyo imeeleza Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isiman, Mkoa wa Iringa amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

“Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo,” amesema Dk Kusiluka.

Lukuvi alikuwa miongoni mwa wabunge waandamizi bungeni ambaye amekuwa mbunge wa Ismani kuanzia mwaka 1995 hadi sasa akihudumu kwa zaidi ya miaka 30.

spot_img

Latest articles

Mgodi wa kihistoria wa niobium kujengwa Mbeya

Na Mwandishi Mbeya TANZANIA imepiga hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Marekani baada...

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

More like this