ETDCO yaahidi kukamilisha Mradi wa Umeme katika vitongoji 372 Ruvuma kwa wakati

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imeahidi kukamilisha kwa wakati mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 372 wenye thamani ya shilingi bilioni 37.9, Mkoani Ruvuma.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya utekelezaji wa mradi huo kati ya ETDCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), iliyofanyika Februari 3, 2026 Mkoani Ruvuma, Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Ahmed Ahmed, ameitaka Kampuni ya ETDCO kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati katika wilaya za Mbinga na Nyasa.

Brigedia Jenerali Ahmed, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa huo, huku akiwahimiza wananchi kujiandaa kuweka miundombinu ya umeme majumbani (wiring) ili waweze kuunganishwa na huduma hiyo mara baada ya mradi kukamilika.

“Ujio wa umeme huo utasaidia kukuza shughuli za kiuchumi na biashara katika maeneo husika,” amesema Kanali Ahmed.

Meneja Usamamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme REA, Mhandisi Deogratius Nagu, amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha wateja takribani 11,914 katika Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO, Mhandisi Richard Mwanja, ameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuipa ETDCO fursa ya kutekeleza mradi huo, huku akieleza kuwa Kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa.

Msimamizi wa Mradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Ali Pandit, amesema kuwa TANESCO imejipanga kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili huduma ya umeme inawafikia wananchi.

Kwa upande wao, Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameipongeza Serikali kupitia REA kwa kuwaletea miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vyao, wakisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

spot_img

Latest articles

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

More like this

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...