Menejimenti ya TMDA yajipanga na Dira 2050

Na Mwandishi Wetu

MENEJIMENTI ya TMDA imekutana Morogoro Februari 2 hadi 3, 2026 kujadili rasimu ya Mpango Mkakati Mpya wa Mamlaka wa miaka mitano, 2026/27-2030/31 unaoakisi utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050.

Rasimu ya Mpango Mkakati huo ni ya Sita kufuatia kukamilika kwa ufanisi kwa Mpango Mkakati wa Tano.

Mpango Mkakati wa Sita wa TMDA unatarajiwa kuanza kutumika mnamo tarehe 01, Julai, 2026.

Pamoja na mambo mengine, rasimu ya Mpango Mkakati husika inalenga katika kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kulinda afya ya Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo, aliwaeleza wajumbe wa kikao husika kuwa rasimu husika ya Mpango Mkakati inabeba Dira mpya ya TMDA ambayo ni “Kuimarika kwa afya na ustawi wa Watanzania wote kupitia udhibiti bora unaokidhi viwango vya kitaifa”.

Dkt. Fimbo aliongeza kuwa, Dhamira Mpya ya Taasisi itakuwa ” Kulinda Afya ya Jamii kwa kuhakikisha, usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa zote zinazohusiana na afya”.

Uongozi wa TMDA umekuwa na utamaduni shirikishi katika kujadili mambo makubwa yahusuyo taasisi, ambapo watumishi wote hushirikishwa kupitia ngazi mbalimbali ndani ya Mamlaka kabla ya kuidhinishwa na Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB).

Pamoja na mambo mengine, Mpango Mkakati huu mpya unaweka mwelekeo wa pamoja katika udhibiti, utasaidia katika kupanga matumizi ya rasilimali vizuri na kuboresha uwajibikaji na uwazi.

Mpango Mkakati wa TMDA ni nyaraka muhimu ambayo inaonesha ramani ya safari ya taasisi na ndiyo chombo muhimu cha kuongoza maamuzi na maendeleo ya TMDA.

spot_img

Latest articles

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

More like this