CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu 

BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini kwa kuweka mifumo ya kifedha itakayowawezesha wabunifu kubadili vipaji vyao na kuwa biashara endelevu zenye mchango wa moja kwa moja katika uchumi wa Taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Jukwaa la Mitindo Tanzania, Meneja wa Huduma kwa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya CRDB, Japhary Hassanal, amesema kuunganisha ubunifu na mifumo ya biashara ni hatua muhimu katika kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya nchi.

“Lengo letu ni kuona ubunifu uliopo unageuzwa kuwa biashara zenye tija, ajira na mchango halisi katika uchumi wa Taifa,” amesema Japhary.

Ameeleza kuwa CRDB inatambua nafasi ya sekta ya mitindo katika kukuza biashara ndogo na za kati, ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kupanua wigo wa uchumi wa ubunifu nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wabunifu Tanzania (FAT), Mustafa Hassanal, amesema tasnia ya mitindo ina uwezo mkubwa wa kuchochea uchumi kupitia viwanda, biashara na diplomasia ya kiuchumi endapo itawekewa mifumo imara na sera rafiki.

“Mitindo leo si suala la urembo pekee, bali ni sekta ya kimkakati inayogusa ajira, biashara na utambulisho wa Taifa,” amesema Hassanal.

Ameongeza kuwa kwa muda mrefu mitindo barani Afrika imekuwa ikionekana kama kipaji kisicho na mifumo madhubuti ya kifedha na kibiashara, hali iliyodhoofisha ukuaji wa sekta hiyo licha ya kuwepo kwa vipaji vingi.

Hassanal amesema Jukwaa la Mitindo Tanzania limeanzishwa ili kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto na kuweka mikakati ya vitendo ya kuigeuza mitindo kutoka kipaji binafsi na kuwa sekta rasmi ya uchumi wa Taifa.

spot_img

Latest articles

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...

More like this

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...