MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi amekutana na wasimamizi wa sheria mbalimbali katika kituo cha Mpaka cha Mutukula, Kagera tarehe 29 Januari, 2026 na kuteta kuhusu masuala ya udhibiti wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika kituo hicho.

Akizungumza na watendaji hao, Mwenyekiti alisema lengo la ziara hiyo ni kujionea shughuli za kiudhibiti maeneo ya Mpakani na kujifunza changamoto zilizopo ili kushauri namna ya kuzitatua.

“Serikali ni moja na yote yanayofanyika yanalenga kuhudumia wananchi, hivyo rai yangu ni kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto za mipakani” , alisema Shitindi.

Akitoa taarifa ya utendaji wa kituo, Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha cha Mutukula, Lubinza Edmund, alisema kituo hicho kina taasisi 20 za udhibiti na jumla ya watumishi ni 116 ambao hufanya kazi kwa ushirikiano katika kubaini magendo na kukabiliana nayo ili kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa salama kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Lubinza aliendelea kuainisha changamoto nyingine kuwa ni ukubwa wa Mpaka ambao una vipenyo vingi, jambo ambalo ni hupelekea bidhaa kuingia kwa kificho hivyo ni lazima watendaji kushirikiana muda wote.

Ziara hiyo katika kituo cha Mutukula, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa MAB, Eric Shitindi ilijumuisha wajumbe wote wa Bodi na Menejimenti ya TMDA ilifanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya Bodi.

spot_img

Latest articles

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...

Al Ahly yaanza safari kuifuata Yanga Zanzibar

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imeanza safari kuelekea Zanzibar kwa...

More like this

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...