TCAA yapokea ugeni kutoka Wizara Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Daniel Malanga, imepokea ugeni wa ziara kikazi kutoka Wizara Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kupata mwanga kuhusu hatua muhimu za kuanzisha shirika la ndege la Zanzibar.

Akizungumza wakati wa kuukaribisha ugeni huo, Januari 20, 2026, katika Makao Makuu ya TCAA, Malanga, alielezea hatua mbalimbali zinazohitajika ili kufanikisha kuanzisha shirika la ndege.

Malanga alisisitiza kuwa hatua hizo ni muhimu ili kuhakikisha shirika la ndege linaanza kazi kwa utaratibu na kwa kufuata sheria za nchi ikiwemo uombaji wa leseni unaoambatanishwa na mpango wa biashara, pamoja na kuzingatia kanuni za udhibiti wa kiuchumi na taratibu nyingine zinazotawala sekta ya usafiri wa anga.

Kwa upande wa wataalamu wa TCAA waliweka wazi masharti ya kuanzisha kampuni ya ndege yanayohusu upatikanaji wa Leseni na Cheti.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar , Mhandisi Ali Said Bakari, alisema lengo la ziara hiyo kulikuwa ni kupata uzoefu wa vitendo na maarifa ya maandalizi ya kuanzisha shirika la ndege. Aidha, aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, iko mbioni kuanzisha shirika la ndege, hivyo wanataka kuelewa kanuni, taratibu na usimamizi wa shirika la ndege ili waweze kuanzisha shirika hilo kwa ufanisi.

Ujumbe huo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ulieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalenga kuanzisha kampuni ya ndege ili kurahisisha usafiri wa anga, hususan kwa watalii wanaoingia na kutoka Zanzibar mara kwa mara. Ilielezwa kuwa mpango huo unalenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar kupitia sekta ya usafiri wa anga, utalii na uchumi wa buluu (Blue Economy).

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa pande zote kueleza dhamira ya kuendelea kushirikiana kwa karibu, ili kuhakikisha mchakato wa uanzishaji wa shirika la ndege unatekelezwa kwa kuzingatia sheria, taratibu na maslahi mapana ya taifa.

spot_img

Latest articles

Yanga yaikung’uta vibaya Mashujaa FC

Na Winfrida Mtoi WANANCHI Yanga wameichakaza timu ya Mashujaa mabao 6-0, huku nyota mpya wa...

Watumishi wapya wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa

Na Mwandishi Wetu, Pwani OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH), kwa kushirikiana na Chuo cha...

Kituo cha kupoza umeme Mtera kuboresha upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza...

Tanesco Kigamboni yatoa elimu y nishati safi ya kupikia shule ya msingi Malaika

Na Mwandishi Wetu KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati...

More like this

Yanga yaikung’uta vibaya Mashujaa FC

Na Winfrida Mtoi WANANCHI Yanga wameichakaza timu ya Mashujaa mabao 6-0, huku nyota mpya wa...

Watumishi wapya wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa

Na Mwandishi Wetu, Pwani OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH), kwa kushirikiana na Chuo cha...

Kituo cha kupoza umeme Mtera kuboresha upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza...