Dawa na vifaa tiba vya Mil. 822.8 vyakamatwa Tabora

Na Mwandishi wetu,TABORA

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Magharibi imefanya oparesheni maalumu na kufanikiwa kukamata dawa zenye thamani ya sh mil 822.8 zilizokuwa zinauzwa kinyume na utaratibu.

Hayo yamebainishwa jana na Meneja wa TMDA Kanda ya Magharibi, Christopher Migoha alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, ambapo alieleza kuwa jumla ya kilo 2,300 zenye thamani ya shilingi mil 822.8 zimekamatwa na kuteketezwa.

Amefafanua kuwa dawa na vifaa tiba hivyo vimekamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika hospitali, vituo vya afya, zahanati na maduka ya dawa baridi za binadamu na mifugo katika Wilaya zote.

Migoha ameeleza kuwa dawa hizo haziruhusiwi kuuzwa katika maduka ya watu binafsi na ni kinyume cha sheria na kanuni ya 63 ya mwaka 2005 ya dawa zilizozuiliwa kuuzwa hadharani hususani katika maduka ya watu binafsi.

Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo walikagua jumla ya maduka 408 ya dawa, Hospital 16, vituo vya afya 17, zahanati 17, famasi 66, maduka ya dawa muhimu za mifugo 37 na maduka ya dawa muhimu za binadamu 230.

Maeneo mengine ni maghala ya kuhifadhi dawa za binadamu 2, kliniki za kibingwa 1, kliniki ya mifugo 1, magari ya kubebea dawa za binadamu na mifugo 20 na maeneo ya uzalishaji maji Tiba 2Aidha ameongeza kuwa walikamata baadhi ya dawa ambazo ni salama lakini hazistahili kuuzwa kwenye maduka hayo na kuzigawa kwenye baadhi ya Hospitali za umma ikiwemo kuondoa sokoni baadhi ya dawa.Migoha amedokeza kuwa mbali na tukio hilo watumishi wa taasisi hiyo pia wamejumuika kwenda kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya sh mil 28.2 kwa hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Milambo iliyoko Mkoani hapa. Naye Afisa Lishe wa Mkoa huo, Paulo Makali, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa huo, amewataka wauzaji na wasambazaji wa dawa kununua dawa kwenye maeneo rasmi ili kuepuka kubabikwa .Baadhi ya wadau wa TMDA, wameshauri kufanyika semina za mara kwa mara kwa wauzaji wa dawa hizo ili kukumbushana juu ya namna bora ya uuzaji wa dawa na vifaa tiba ili kuokoa afya za watumiaji.

spot_img

Latest articles

Kata za Mzinga, Malangali kupiga kura kuchagua madiwani kesho

Na Mwandishi wetu, Dodoma JUMLA ya Wapiga Kura 38,151 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la...

TCAA yapokea ugeni kutoka Wizara Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi...

Yanga yaikung’uta vibaya Mashujaa FC

Na Winfrida Mtoi WANANCHI Yanga wameichakaza timu ya Mashujaa mabao 6-0, huku nyota mpya wa...

Watumishi wapya wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa

Na Mwandishi Wetu, Pwani OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH), kwa kushirikiana na Chuo cha...

More like this

Kata za Mzinga, Malangali kupiga kura kuchagua madiwani kesho

Na Mwandishi wetu, Dodoma JUMLA ya Wapiga Kura 38,151 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la...

TCAA yapokea ugeni kutoka Wizara Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi...

Yanga yaikung’uta vibaya Mashujaa FC

Na Winfrida Mtoi WANANCHI Yanga wameichakaza timu ya Mashujaa mabao 6-0, huku nyota mpya wa...