Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi ili kufanikisha maendeleo ya kweli.

Salome ameyasema hayo Januari 8, 2026, mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati inayotekelezwa mkoani humo.

Amesema wananchi wana imani kubwa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa viongozi kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinatatuliwa kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika siku 100 za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Wizara ya Nishati imejipanga kuhakikisha umeme unawashwa kwenye miradi ya vitongoji mkoani Shinyanga ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Salome ametembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ambapo alikutana na Katibu wa CCM Mkoa huo pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) sambamba na Sekretarieti ya Mkoa ambapo amesema kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Chama na Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake, Odilia Abraham Batimayo alisifu utendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kwa kushughulikia kero na changamoto za wananchi kwa wakati, hatua inayochangia kujenga imani kwa wananchi kwa Serikali yao.

Salome yuko mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwemo mradi wa umeme wa jua wa Kishapu pamoja na miradi ya umeme wa vitongoji katika vijiji mbalimbali vya mkoa huo.

spot_img

Latest articles

2025 mwaka wa mageuzi na matokeo katika mashirika ya umma

Na Mwandishi Wetu MWAKA 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Ofisi ya Msajili wa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...

Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu...

Serikali yawekeza zaidi ya Sh. Bilioni 280 kuimarisha upatikanaji umeme Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano...

More like this