Aweso aridhishwa na wingi wa maji Ruvu Juu, aipa Dawasa jukumu

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa maji, Jumaa Aweso amekagua na kujiridhisha na wingi wa Maji yanayoingia katika Mtambo wa Maji Maji Ruvu Juu uliopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ikiwa ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa huduma ya Maji.

Aweso amesema hatua hiyo ni jitihada zinazoendelea kutekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na Taasisi za DAWASA na Bonde la Wami Ruvu za kuhakikisha inapambana na upungufu wa huduma ya maji iliyojitokeza katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Nimeona kazi inayoendelea niseme kwa dhati nimefarijika na inanipa imani kubwa kwamba tutavuka salama katika kipindi hiki cha mpito, niwapongeze watu wa DAWASA, Bonde la Wami Ruvu, vyombo vya ulinzi na Usalama pamoja na wadau wote wanaoshiriki kazi hii kuhakikisha inakamilika kwa wakati” ameeleza Waziri Aweso.

Amesema kuwa maendeleo ya kazi hiyo ni hatua muhimu katika jitihada za kuwapatia huduma endelevu ya maji wananchi wa Dar es Salaam na Pwani na kuendelea kuwaasa Wananchi kutumia maji kwa uangalifu na kuwa na desturi ya kuwa na vyombo vya kuhifadhi Maji.

“Tumepokea habari njema kutoka kwa wenzetu wa Mamlaka ya hali ya hewa kuwa mvua zinaanza kunyesha, na tayari katika maeneo ya Morogoro mvua imenyesha siku ya jana, nina imani kubwa tutavuka salama kipindi hiki cha mpito na hali kurejea sawa. Katika kipindi hiki tutahakikisha maji yanayopatikana yanagawanywa kwa usawa kwa kila mwananchi” amesisitiza Aweso.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this