Waziri Aweso aweka kambi Dar kupambana na changamoto upungufu wa maji

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kwa kutembelea matanki makubwa ya uhifadhi Maji, mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini ili kujionea hali ilivyo ya uzalishaji maji na usambazaji Ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Maji kupunguza changamoto ya upungufu wa Maji uliojitokeza kutokana na kuchelewa kwa mvua.

Waziri Aweso amewasihi Wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na vyombo vya kutunza na kuhifadhi maji katika kipindi hiki na ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kushirikiana na wadau binafsi wenye visima vikubwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

Pia Waziri Aweso ameongeza kwa kutoa maagizo kwa DAWASA kuhakikisha visima vyote vilivyochimbwa na Serikali vinaingizwa kwenye mfumo wa usambazaji ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa Wananchi.

spot_img

Latest articles

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

More like this

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...