Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu amejiuzulu nafasi ya makamu mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Machumu amekabidhi barua ya kujiuzulu kwake kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, leo Jumatano Novemba 26, 2025 alipokutana na wahariri kwenye kikao cha ndani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amesema kwa nafasi yake mpya anaona kutakuwa na mgongano wa masilahi na wadhifa huo.
Baada ya kupokea barua hiyo, Balile amekubali kujiuzulu kwa Machumu na kuwa Kamati ya Utendaji ya TEF itakaa baadaye leo kujadili suala hilo.
Machumu aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu.


