Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi limesema limeona na linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya (OCD), mkoani Mbeya kwa waandishi wa habari kama ushauri kwa wamiliki wa vituo vya mafuta wilayani humo.
Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Jeshi hilo leo Novemba 26,2025, imesema uchunguzi unafanyika ili kupata ukweli wa taarifa hiyo, kwani hana mamlaka ya kuita waandishi wa habari na kutoa taarifa kwao. “Ikibainika hivyo hatua stahiki zitachukuliwa mara moja.
Mapema leo ilisambaa video ikimuonesha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya (OCD), akitoa angalizo kwa wauzaji wa mafuta katika Wilaya hiyo, pamoja na kuwataka wasiwauzie madereva wa bodaboda mafuta yanayozidi lita mbili kwa wakati mmoja kuelekea Desemba 9, 2025.


