Waziri Mkuu atoa sababu yakutotaja idadi vifo vilivyotokea Oktoba 29

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema ni muhimu watanzania kutanguliza utu na heshima kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, akipinga namna ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakichapisha taarifa au picha mtandaoni kana kwamba vifo ni jambo la kusherehekewa.

Amesema hayo wakati akijibu maswali aliyoulizwa  kwenye mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ya kutaka kujua idadi ya vifo vilivyotokea Oktoba 29, 2025  kutokana na maandamano yaliyofanyika na kusababisha vurugu.

“Tunaongelea maisha ya watu, tunaongelea watu waliopoteza wapendwa wao. Mtu amepoteza ndugu yake halafu wewe unaposti kama hafla,” amesema Waziri Mkuu, akionyesha masikitiko yake juu ya tabia ya kutafuta umaarufu kupitia misiba.

“Katika mazingira ambayo mtu amepoteza mpendwa wake mnataka tuanze kuhesabu kama majengo, magari au mafanikio? Mwingine anataja idadi licha ya kwamba hayupo hapa,” ameeleza.

Aidha Dk. Mwigulu ametaja  vitu vilivyoharibiwa  kutokana na vurugu hizo kuwa ni magari 1,642 ya watu binafsi yaliharibiwa, baadhi yakiteketezwa kwa moto, vituo vya mafuta 672 na bodaboda 2,268.

Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia utulivu na amani, akibainisha kuwa Watanzania wanapaswa kuepuka fujo zinazoweza kuharibu maisha na ustawi wa kila mmoja.

Ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na makundi ya watu wenye nia ya kuichafua na kuiharibu Tanzania na wakatae kutumiwa kufanya uovu.

“Kila mmoja alibebe jambo hili kwa ukubwa, hawatupendi, wanaangalia rasilimali zetu, nchi yetu sio masikini, kuna watu wanamezea mate rasilimali zetu, ninawahakikishia kuwa tutailinda Tanzania na Rasilimali zake kwa gharama yoyote ile,”

spot_img

Latest articles

Niffer arudishwa gerezani, 20 kesi ya uhaini waachiwa huru

Na Mwandishi Wetu Watuhumiwa 20 kati ya 22 waliokuwa wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini wameachiwa...

Dk.Mwigulu aagiza Kanisa Gwajima lifunguliwe

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na...

Ndejembi asisitiza ushirikiano kwa viongozi katika utekelezaji wa miradi yenye kipaumbele kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi (Mb), ametoa wito kwa viongozi na...

Naibu Waziri Nishati, akutana na Menejimenti ya Ewura, aitaka kuongeza kasi na ufanisi zaidi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, leo tarehe 24.11.2025 amekutana na...

More like this