Naibu Waziri Nishati, akutana na Menejimenti ya Ewura, aitaka kuongeza kasi na ufanisi zaidi

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, leo tarehe 24.11.2025 amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo hivi karibuni.

Makamba amekutana na viongozi hao kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya utendaji na maboresho ya sekta ya nishati nchini.

Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya EWURA jijini Dodoma.

Aidha, ameipongeza EWURA kwa kazi nzuri katika kusimamia huduma za nishati, na kuitaka Mamlaka hiyo kuongeza kasi, ubunifu na ufanisi.

“Mimi si muumini wa kushindwa, hivyo natoa rai kwenu kujipanga ili kuendana na kasi hiyo, ili muendelee kung’ara katika uendeshaji wa shughuli zenu” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, aliwasilisha mbele ya Makamba taarifa fupi kuhusu majukumu ya Mamlaka, mafanikio yaliyopatikana, pamoja na maeneo yanayoendelea kuimarishwa.

Dkt. Andilile aliahidi taasisi yake kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na za uhakika.

spot_img

Latest articles

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

More like this

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...